|
Nyanja za kazi
|
ANCOSO Development GmbH ni kampuni inayopanuka na iliyo na makazi yake kwenye jimbo la Leipzig, Sachsen na Uswisi. Tunaendeleza na kuuza bidhaa mbalimbali za utatuzi wa Usimamizi wa Yaliyomo, usimamizi wa nakala, mtiririko wa kazi za biashara, ushirikiano na usimamizi aw wafanya kazi hadi uhusishaji wa washirika. Kwa sasa tuna wafanya kazi 7 Sachsen na 15 katika Uswisi. Tunafanya yafuatayo kuiongezea timu yetu nguvu: Wao huendeleza vifaa vya kisasa na vizuri kwa watumizi kupitia IBM WebSphere wakiwa katika kikundi kidogo. Muondoko wetu wa kushirikiana na kutozingatia mamlaka ya wafanya kazi itakupa fursa nzuri ya kufanya kazi kwa ubunifu.Wakiwa mojawapo ya timu bunifuna yenye uhodari, wao huendeleza vifaa hivyo wakitumia njia za kisasa zaidi za uendelezaji, na kupitia kwa teknolojia J2EE na vipokezi vya matumizi vya WebSphere, Jboss na Tomcat.
|
|
Tunayokuahidi
|
Licha ya kujaribu kwetu kukuza mahitaji ya bidhaa zetu katika soko linalopanuka, tunakuahidi malipo sambamba na utendaji wako, fursa ya kujiendeleza, ushirikiano wa kuvutia na kazi ya kujiongoza katika timu changa. Tunawapa wenzetu waliojibidiisha zaidi fursa ya kujiunga moja kwa moja na hisa zetu anzilishi kwa idadi ya asilimia 2 kufikia 5. Hivyo waweza kujumuika moja kwa moja kwenye ukuzaji mwepesi wa raslimali za kampuni. Uendelezaji huru wa kazi pia unawezekena kupitia ombi.
|
|
masomo
|
Umehitimu masomo katika uwanja wa teknolojia ya mawasiliano au mwingine unaokaribiana na huu. Unao ujuzi wa kuunda programu ukitumia Portlets chini ya WebShere lango la 5 au 6, una ujuzi wa kutosha katika Java, unajua kijerumani na kiingereza na uko tayari kufanya kazi pia na wateja wetu waswisi.
|